TAARIFA KWA UMMA: KUTANGAZA MATOKEO "IPO" YA DSE

TAARIFA KWA UMMA:
KUTANGAZA MATOKEO YA UUZWAJI WA AWALI (IPO)
WA HISA 15,000,000 ZA
DAR ES SALAAM STOCK EXCHANGE PLC (DSE)

 

Kampuni ya Dar es Salaam Stock Exchange PLC (DSE) iliendesha mauzo ya awali (IPO) kuanzia Jumatatu tarehe 16 Mei 2016 hadi Ijumaa tarehe 3 Juni 2016 kwa matarajio ya kuzalisha mtaji wa TZS 7,500,000,000 kutokana na mauzo ya hisa 15,000,000 kwa bei ya TZS 500/= kwa hisa moja.
Matokeo ya mauzo ya awali yanaonyesha DSE imefanikiwa kuzalisha mtaji wa TZS 35,768,796,000 na kupitiliza kiwango cha mtaji kilichopangwa kwa asilimia 377%.
Zoezi la mauzo ya awali litafuatiwa na marejesho kwa wawekezaji ya fedha zilizozidi kiwango cha mtaji kitakachoshauriwa na mamlaka ya masoko ya mitaji (CMSA).
Mauzo ya hisa na kujiorodhesha katika soko la hisa la Dar es Salaam inafuatia mahitaji ya kisasa ya masoko ya hisa na yamekusudiwa kuleta ubora na tija katika utendaji wa uongozi wa DSE na zaidi katika kuimarisha utekelezaji wa mikakati na utendaji wake.
 
Ratiba ya Matukio Muhimu  
Tukio  Tarehe
Kuanza kwa Mauzo 16 Mei 2016
Kufunga Mauzo 03 Juni 2016
Ugawaji wa Hisa 10 Juni 2016
Kutangaza Matokeo 16 Juni 2016
Kusajilisha Akaunti za CSD 24 Juni 2016
Kuratibu hundi za malipo 30 Juni 2016
Kujiorodhesha na Kuanza Mauzo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam 12 Julai 2016
 
Kwa taarifa zaidi, tafadhali rejea nakala ya muhtasari wa kampuni ya DSE unaopatikana kwenye tovuti yetu ya www.dse.co.tz.
 
Imetolewa na:
 
Menejimenti
Dar es Salaam Stock Exchange PLC